Katika kusherekea siku ya Wanawake Duniani, tarehe 08/03/2024 wanawake wa NIMR kituo cha Tanga walitoa huduma ya upimaji wa afya na matibabu kwa wananchi wa Tanga mjini. Vile vile walitembelea Gereza la Maweni kutoa misaada na kuwafariji wafungwa Wanawake.